Romans 3:9-19

Wote Wametenda Dhambi

9 aTusemeje basi? Je, sisi ni bora kuwaliko wao? La hasha! Kwa maana tumekwisha kuhakikisha kwa vyovyote kwamba Wayahudi na watu wa Mataifa wote wako chini ya nguvu ya dhambi. 10 bKama ilivyoandikwa:

“Hakuna mwenye haki, hakuna hata mmoja.
11Hakuna hata mmoja mwenye ufahamu,
hakuna hata mmoja amtafutaye Mungu.
12 cWote wamepotoka,
wote wameoza pamoja;
hakuna atendaye mema,
naam, hakuna hata mmoja.”
13 d“Makoo yao ni makaburi wazi;
kwa ndimi zao wao hufanya udanganyifu.”
“Sumu ya nyoka iko midomoni mwao.”
14 e“Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.”
15 f“Miguu yao ina haraka kumwaga damu;
16maangamizi na taabu viko katika njia zao,
17 gwala njia ya amani hawaijui.”
18 h“Hakuna hofu ya Mungu machoni pao.”
19 iBasi tunajua ya kwamba chochote sheria inachosema, inawaambia wale walio chini ya sheria ili kila kinywa kinyamazishwe na ulimwengu wote uwajibike kwa Mungu.
Copyright information for SwhNEN